Friday, November 15, 2013

MWANAMUZIKI WA AKUDO IMPACT AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA HUKO NCHINI CHINI,,,,,,BONYEZA HAPA UIPATE STORY NZIMA

wimbi la vijana wengi kutoka nchini tanzania kukamatwa nje ya nchi kwa kukutwa na madawa ya kulevya linazidi kushika kasi baada ya juzi mwanamuziki wa akudo impact ambae kiasili anatoka jamhuri ya kidemokrasi ya congo kukamatwa na unga{MADAWA}

taarifa kutoka china zinasema kuwa mwanamuziki huyo anaejulikana kwa jina la CANAL TOP ambae ni muimbaji na rapper wa bendi hiyo amekutwa na mzigo huo katika uwanja wa ndege jijini beijing china huku pasport yake ikionyesha kuwa ametoka jijini daresalaam TZ.
tukio hili linafanya kuwepo na msururu mrefu wa watanzania waliokamatwa nje ya nchi huku wengine tayari wakiwa wamehukumiwa kunyongwa na vifungo vya miaka mingi ughaibuni

wito wetu ni kuwaasa vijana wenzetu kuepuka matumizi ama usafirishaji wa madawa hayo ambayo yamekuwa ni chanzo cha vijana wengi kuharibikiwa na wengine kuwasababishia vifo.

Wednesday, August 28, 2013

KAGAME,MUSEVEN,KENYATA,WAANZA MIPANGO YA KUIMALIZA TANZANIA KIUCHUMI

HATIMAE ULE MPANGO WA RAIS WA RWANDA PAUL KAGAME WA KUACHA KUITUMIA BANDARI YA DARESALAAM SASA UMECHUKUA SURA MPYA.
HATUA HIYO INAFUATIA UZINDUZI WA KUIFANYA BANDARI YA MOMBOSA KUWA BANDARI KUBWA NA YA KISASA ZAIDI UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI NA KATI

HAYA YAMETOKEA JUZI BAADA YA MARAIS WA NCHI TANO KUKUTANA NCHINI KENYA KUZINDUA MPANGO HUO
MARAIS WALIOKUTANA NI PAUL KAGAME WA RWANDA,SALVAKIYR WA SYDAN KUSINI,PIER NKURUNZINZA WA BURUNDI,YOWERI MUSEVEN WA UGANDA NA UHURU KENYATTA WA KENYA.
MPANGO HUO UMEKUJA KUFUATIA KAULI YA KAGAME NA MUSEVEN KUDAI KUWA KUANZIA TAREHE 1SEPTEMBER HAWATATUMIA TENA BANDARI YA DARESALAAM KUTOKANA NA KUTOKUWA NA UHUSIANO MZURI BAINA YAO NA RAIS KIKWETE,

HIVYO KUAMUA KUWA KWA VILE BANDARI YA DAR NI CHANZO KIKUU CHA PATO LA TAIFA BASI WAO KAMA WATUMIAJI WAKUBWA HAWATAITUMIA TENA BANDARI HIYO NA KUAMUA KUWEKEZA BANDARI YA MOMBASA AMBAPO KATIKA MIPANGO HIYO NI KUBORESHA  GATI NO 19 PAMOJA NA UJENZI WA NJIA ZA RELI ZITAKAZOKUWA ZIKIENDA MOJA KWA MOJA KATIKA NCHI HIZO.
BAADHI YA WANADIPLOMASIA WAMEZUNGUMZIA HATUA HIYO NA KUSEMA KUWA WANA WASI WASI NA MUUNGANO WA SHIRIKISHO LA AFRIKA MASHARIKI  KAMA LITADUMU KWA SABABU HATA NDANI YA BUNGE LA EAC KUMEKUWA NA KUTOELEWANA KATIKA SIKU ZA HIVI KARIBUNI.

Saturday, July 13, 2013

KESHO NDIO KESHO UCHAGUZI MDOGO WA MADIWANI ARUSHA KUFANYIKA

Kesho ndio ile siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kwa wakazi wa kata 4 ambazo uchaguzi wake uliahirishwa hapa jijini arusha kufuatia mashambulio ya mabom kkutoka kwa watu ambao bado hawajajulikana mpaka sasa

katika kumalizia siku ya mwisho kwa kampeni za chini chini kila chama kimekuwa kikifanya jitihada mbalimbali huku kukiwa na kulaumiana kwa kila upande,
CCM wamekuwa wakifanya kampeni zinazoongozwa na mh MWIGULU NCHEMBA.
Na kwa upande wa chadema kumekuwa na timu inayofanya kampeni za mwisho mwisho ambapo jioni hii kumekuwa na taarifa zilizotolewa na chadema kuwa,baadhi ya wafuasi wa ccm wakiongozwa na mwigulu wameonekana wakigawa sare za combat zinazotumiwa na chadema ili kuwavalisha baadhi ya vijana ionekane kama ni wafuasi wa chadema na bahati mbaya mchezo mzima wao chadema wameushtukia na kuripot polisi jioni hii,,
hali ni tulivu saana mjini arusha hakuna vurumai yoyote iliyoripotiwa mpaka sasa na wakazi wa kata hizo wameombwa kufanya uchaguzi wa salama na amani ili kudumisha amani yetu.



Wednesday, April 3, 2013

akamatwa akiiba bata wa jirani na kuvunjwa miguu yote-ni hapa arusha daraja mbili