Friday, November 15, 2013

MWANAMUZIKI WA AKUDO IMPACT AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA HUKO NCHINI CHINI,,,,,,BONYEZA HAPA UIPATE STORY NZIMA

wimbi la vijana wengi kutoka nchini tanzania kukamatwa nje ya nchi kwa kukutwa na madawa ya kulevya linazidi kushika kasi baada ya juzi mwanamuziki wa akudo impact ambae kiasili anatoka jamhuri ya kidemokrasi ya congo kukamatwa na unga{MADAWA}

taarifa kutoka china zinasema kuwa mwanamuziki huyo anaejulikana kwa jina la CANAL TOP ambae ni muimbaji na rapper wa bendi hiyo amekutwa na mzigo huo katika uwanja wa ndege jijini beijing china huku pasport yake ikionyesha kuwa ametoka jijini daresalaam TZ.
tukio hili linafanya kuwepo na msururu mrefu wa watanzania waliokamatwa nje ya nchi huku wengine tayari wakiwa wamehukumiwa kunyongwa na vifungo vya miaka mingi ughaibuni

wito wetu ni kuwaasa vijana wenzetu kuepuka matumizi ama usafirishaji wa madawa hayo ambayo yamekuwa ni chanzo cha vijana wengi kuharibikiwa na wengine kuwasababishia vifo.

No comments:

Post a Comment