Kesho ndio ile siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kwa wakazi wa kata 4 ambazo uchaguzi wake uliahirishwa hapa jijini arusha kufuatia mashambulio ya mabom kkutoka kwa watu ambao bado hawajajulikana mpaka sasa
katika kumalizia siku ya mwisho kwa kampeni za chini chini kila chama kimekuwa kikifanya jitihada mbalimbali huku kukiwa na kulaumiana kwa kila upande,
CCM wamekuwa wakifanya kampeni zinazoongozwa na mh MWIGULU NCHEMBA.
Na kwa upande wa chadema kumekuwa na timu inayofanya kampeni za mwisho mwisho ambapo jioni hii kumekuwa na taarifa zilizotolewa na chadema kuwa,baadhi ya wafuasi wa ccm wakiongozwa na mwigulu wameonekana wakigawa sare za combat zinazotumiwa na chadema ili kuwavalisha baadhi ya vijana ionekane kama ni wafuasi wa chadema na bahati mbaya mchezo mzima wao chadema wameushtukia na kuripot polisi jioni hii,,
hali ni tulivu saana mjini arusha hakuna vurumai yoyote iliyoripotiwa mpaka sasa na wakazi wa kata hizo wameombwa kufanya uchaguzi wa salama na amani ili kudumisha amani yetu.
